Polisi Tanzania: Wengi wanaoripotiwa kutekwa hujificha kwa sababu binafsi
Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatano tarehe 18 Juni 2025, ambayo imeeleza baadhi ya matukio hayo, polisi wamesema uchunguzi wa kina umebaini kuwa watu wengi waliodaiwa kutekwa ama walikuwa wamejificha kwa hiari, walitoroka kutokana na sababu mbalimbali au walihusika katika vitendo vya uhalifu kabla ya kupotea kwao.