Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Watu 4,000 wamefariki dunia kwa ajali za barabarani nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu - Mwanzo TV

Watu 4,000 wamefariki dunia kwa ajali za barabarani nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitatu

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Zaidi ya watu elfu nne wamefariki dunia katika ajali za barabarani katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, huku wengine zaidi ya elfu tano wakijeruhiwa katika ajali hizo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa takwimu hizo huku akielezea kuwa hazifurahishi, kutokana na kuchukua uhai wa Watanzania licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali za kuboresha barabara hapa nchini.

Akifungua maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yanayofanyika Kitaifa mkoani Mwanza, Waziri Mkuu Majaliwa amesema elimu zaidi na udhibiti wa madereva inapaswa kuongezwa, ili kupunguza ajali zinazoendelea kuchukua uhai wa Watanzania.

Ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kutumia teknolojia za kisasa katika kudhibiti ajali za barabarani, ikiwa ni pamoja na kutambua madereva wanaovunja kwa makusudi sheria za babarani na kusababisha ajali.

Waziri Mkuu Majaliwa ametaka umakini kwa wamiliki wa mabasi yanayoenda masafa marefu, na kuhakikisha kunakuwa na madereva wawili katika kila basi linaloenda masafa marefu.