Chama kipya cha The Equitable Party (TEP) kinachoongozwa na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kimefanikiwa kusajili wanachama zaidi ya milioni moja katika kipindi cha saa 24 tangu kuzinduliwa kwake, kutoka wanachama takriban elfu 30 wakati wa uzinduzi siku ya Jumapili.
Katika taarifa, TEP imesema ongezeko hilo limetokana na hatua ya wakenya waliojiuzulu kutoka vyama vingine vya kisiasa na kujiunga na chama hicho, huku kikianza kujiimarisha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2027.
Kulingana na msemaji wa Linda Mwananchi Caroli Omondo, chama hicho kimeeleza kuwa mfumo wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) huenda uko a changamoto ila wakenya wameendelea kujiunga nacho kwa wingi.
“Huenda mfumo wa ORPP Kenya umekabiliwa na tatizo la uandikishaji lakini wananchi bado wanajiandisha kwa wingi kama wanachama wetu,” Omondi.
TEP ilisema zoezi la kuandikisha wananchama limeendelea kwa kasi, ikieleza kuwa ongezeko hilo ni ishara tosha kwamba wakenya wanatafuta mwelekeo mpya wa kisiasa wenye usawa zaidi.
Chama hicho kimewahimiza wakenya ambao bado hawajajiunga kujisajili kwa kubonyeza *509# kisha kufuata maelekezo ya kujiunga na chama cha kisiasa alafu kuingiza msimbo za chama 100.
Chama hicho pia kilisema usajili unaweza kufanyika kupitia mfumo wa eCitizen au Mfumo Jumuishi wa usimamizi wa Vyama vya Kisiasa (IPPMS) mtandaoni.
TEP ilisema wanachama wapya watapokea nambari za usajili zinazoanza na “TEP-XXXXXXXX”, ambazo baadaye zitabadilishwa kuwa “LMM-XXXXXXXX” mara tu mchakato wa kubadilisha chapa ya chama kuwa Linda Mwananchi Movement (LMM) utakapokamilika.
Ongezeko hilo la wanachama lililoripotiwa na chama hicho linajiri baada ya Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kutangazwa kuwa kiongozi na mgombea wake wa urais wakati wa hafla iliyofanyika jijini Nairobi Jumapili, Oktoba 4, 2026.
TEP inahusishwa na Linda Mwananchi Movement, muungano uliowaleta pamoja viongozi kadhaa wa kisiasa huku wakijiandaa kwa uchaguzi mkuu wa 2027.
Uzinduzi huo umefungua ukurusa mpya kwa Sifuna na wandani wake wanapojitahidi kuimarisha miundo ya chama na kukiweka tayari kwa uchaguzi ujao.
Kupitia kaulimbiu “Tusawazishe” inalenga kuweka usawa wa fursa, heshima na utu sawa, pamoja na kujenga Kenya inayowahudumia wengi badala ya wachache.
Wakati wa uzinduzi huo, Sifuna aliahidi kuiondoza TEP Kkwa uadilifu na nidhamu ya kisiasa anapojiandaa kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Seneta huyo wa Jimbo la Nairobi alisema hicho kitaweka mkazo katika mabadiliko na uongozi unaomweka mwananchi mbele, akisema huo ndio utakuwa suluhu kwa baadhi ya chanagmoto za kisiasa zinazoikabila Kenya.
“Tunaamini katika usawa wa fursa kwa kila mtu katika taifa hili. Tutasikiliza kabla ya kuzungumza, tutashauriana kabla ya kufanya maamuzi na kutaeleza sera zetu na kuwajibika kwa kila hatua tunayochukua,” Sifuna alisema.








