Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
UAE yatangaza wikendi ya Jumamosi na Jumapili na siku nne na nusu za kazi. - Mwanzo TV

UAE yatangaza wikendi ya Jumamosi na Jumapili na siku nne na nusu za kazi.

Milki za Kiarabu imetangaza Jumanne kwamba wiki ya kazi itakuwa siku nne na nusu, ikiwa ni Ijumaa alasiri, Jumamosi, na Jumapili kuunda wikendi mpya. Idara zote za serikali ya Shirikisho zitahamia kwa wikendi hii mpya kuanzia Januari 1, 2022.

Mamlaka iliongeza kuwa kutokana na hatua hii UAE imekuwa taifa la kwanza duniani kuanzisha wiki ya kazi iliyo fupi kuliko wiki ya kawaida ya siku tano kama ilivyo kwa mataifa mengine.

Wiki ya kazi itaanza Jumatatu na kumalizika Ijumaa alasiri. Saa za kazi kwa wafanyakazi wa shirikisho zitaanza saa 1:30 hadi saa 9:30, ikiwa ni jumla ya saa 8.5 za kazi kwa siku. Siku ya Ijumaa, wafanyikazi watafanya kazi kwa saa 4.5 pekee.

Siku ya Ijumaa, wafanyakazi pia wataruhusiwa kuchagua iwapo watafanya kazi kutoka nyumbani au ofisini. Kulingana na serikali ya shirikisho, wikendi ndefu inalenga kuongeza tija na kuboresha usawa wa maisha ya familia na kufikia kiwango kikubwa cha utendaji wa kukuza uchumi wa nchi.