Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Waziri Mkuu wa Australia atahadharisha ushiriki wa Rais Putin kwenye mkutano wa G20 - Mwanzo TV

Waziri Mkuu wa Australia atahadharisha ushiriki wa Rais Putin kwenye mkutano wa G20

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema hii leo kwamba mpango wa Rais Vladmir Putin wa Urusi wa kutaka kushiriki mkutano wa kilele wa kundi la nchi tajiri na zinazoinukia kiuchumi la G20 licha ya kushuhudiwa mgogoro wake na Ukraine, ni hatua ya kuvuka mpaka. 

Mkutano huo utafanyika baadae mwaka huu huko nchini Indonesia. Morrison amewaambia waandishi habari mjini Melbourne kwamba uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ni hatua ya kimabavu na ukiukaji wa sheria ya kimataifa na kwa hivyo fikra ya kukaa kwenye meza moja na Putin ni hatua ya kuvuka mipaka. 

Amesema tayari Marekani iko katika mwelekeo wa kuutaja uvamizi wa Ukraine kuwa uhalifu wa kivita. 

Jana waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema Marekani imebaini kwamba vikosi vya Urusi vimefanya uhalifu wa kivita ndani ya Ukraine akisema nchi hiyo iliwalenga makusudi raia na kutumia mbinu za kivita zilizoshuhudiwa Chechnya na Syria.