Mahakama ya Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa, imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Kitelewasi, Godi Waya (30) kifungo cha maisha baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka saba (jina linahifadhiwa).
Godi ambaye aliajiriwa kulisha ngâombe wa bibi wa mtoto huyo alidaiwa kumtoa mwathirika chumbani kwake na kumpeleka chumba anacholala na kuanza kumbaka huku akiwa amemziba mdomo na kumtisha asimwambie mtu alichofanyiwa.
Hakimu Mkazi Edward Uphoro alikataa utetezi wa mshtakiwa huyo kuwa alibambikiwa kesi hiyo. Amesema kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwa yeye ndiye aliyefanya kitendo hicho na mwathirika alionekana akitoka chumbani kwake akiwa uchi.
âSuala la kubambikiwa kesi halina mashiko kwa sababu kuna ushahidi wa kimazingira na mshtakiwa mwenyewe alikiri mahakamani kuwa mtoto huyo alitoka chumbani na kwamba alikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwake. Swali ni je, kwa nini alitoka akiwa uchi?
âMahakama hii imejiridhisha kuwa ushahidi uliotolewa na mwathirika pamoja na bibi yake ulikuwa na uzito wa kumtia mtuhumiwa hatiani kwa kosa la kulawiti,â amesema
Hakimu huyo amesema mahakama inatoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye matamanio kama hayo kwani vitendo hivyo vimekithiri katika jamii na kusababisha watoto kuishi kwa wasiwasi katika mazingira yanayowazunguka.
“Vitendo hivi vimekuwa vikisababisha watoto kuharibika na kuwa mashoga, hivyo, mahakama hii inatoa adhabu kali ya kifungo cha maisha kwa Godi Waya ili iwe fundisho kwa jamii kuhusu vitendo hivi,” amesema.