Uchaguzi mdogo wa Ubunge kufanyika kesho Mbarali
Kwa mujibu wa taarifa ya NEC iliyotolewa leo ni kwamba uchaguzi wa jimbo hilo la Mbarali unakwenda sambamba na mchakato wa kata sita za Tanzania Bara ambao utahusisha vituo 580 vya kupigia kura.
Kwa mujibu wa taarifa ya NEC iliyotolewa leo ni kwamba uchaguzi wa jimbo hilo la Mbarali unakwenda sambamba na mchakato wa kata sita za Tanzania Bara ambao utahusisha vituo 580 vya kupigia kura.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael kuwahimiza Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kuwalipa watumishi wa Afya stahiki zao kwa wakati.
Leo imetimia miaka sita katika historia ya maisha ya mwanasiasa na mwanasheria nguli nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye sasa amepata ulemavu wa kudumu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana siku kama ya leo Septemba 7,2017 jijini Dodoma kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu
Rais Samia ameeleza hayo leo Ikulu ndogo ya Visiwani Zanzibar wakati akiwaapisha vingozi wateule aliowateua Agosti 30,2023 ambapo pamoja na mambo mengine ameweka msisitizo wake kwa aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mchengerwa ambaye sasa amehamishiwa katika Wizara ya Tamisemi kuhakikisha anacheza karata zake vizuri ili ushindi urudi kwenye serikali yake.
Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya imemhukumu kifungo cha maisha jela Ezekia Mwaitoto Msawile (45) mkazi wa Ilemi jijini Mbeya baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili ya unajisi na kumwingilia kinyume cha maumbile mtoto wa miaka tisa.
Tanzania inajiandaa kufanya kampeni ya utoaji wa chanjo ya Polio Virus 2 (CVDPV2) katika Mikoa 6 inayopakana na nchi za Zambia na Burundi ambapo zoezi hilo limepangwa kufanyika mwezi Septemba na Novemba Mwaka huu 2023 ili kuwakinga watoto.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu leo Agosti 30, 2023 imebainisha kuwa Rais Samia amefuta Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na badala yake ameunda wizara mpya mbili ambazo ni Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Uchukuzi.
Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru Mkoani Mbeya imewafikisha mahakamani watu 14 wakiwemo watumishi wa Halmashauri mbalimbali mkoani humo wakituhumiwa kwa makosa 16 ikiwemo kuendesha genge la uhalifu na utakatishaji wa fedha zaidi ya shilingi Million 350.
Kukamatwa kwa watu hao kumekuja siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutaja ubadhilifu wa fedha mkoani Mbeya
Ubalozi huo umetoa ufafanuzi ikiwa ni siku mbili tangu taarifa hizo zilizodai Sayuni aliyedaiwa kunyanyang’anywa hati ya kusafiria na mwenyeji wake kuwa alikosa huduma ubalozini hapo na kumtaka arudi ajaze maombi hayo kwa njia ya mtandao