Tanzania kuhakiki Makala ya CNN iliyofichua Mauaji ya Uchaguzi Mkuu
Serikali ya Tanzania imesema inafatilia kwa ukaribu makala mpya ya televisheni ya kimataifa ya CNN, ambayo imeeleza kwa kina madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu na matukio ya vifo vya watu wakati wa maandamano yaliyofuatia uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.