Watano Wafariki dunia, Saba hawajulikani Walipo Kufuatia Maporomoko ya Ardhi Indonesia
Takriban watu watano wameripotiwa kufariki dunia kufuatia mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yaliyoikumba kisiwa kikuu cha Java nchini Indonesia mapema wiki hii, shirika la maafa la kitaifa lilisema Ijumaa, wakati waokoaji wakikimbia kutafuta wengine saba ambao bado hawajulikani walipo.