Watuhumiwa wa ubakaji wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu Iringa wadakwa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa limewakamata watuhumiwa watano wa unyang’anyi kwa kutumia silaha ambao kati yao wawili wametambuliwa kuhusika katika tukio la ubakaji alilofanyiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa (jina linahifadhiwa) wakati wakifanya uharifu chuoni hapo.