WHO:Watu milioni 8 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tumbaku
Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula.