Wasira:Tusahau mchakato wa uchaguzi, sasa tuungane kusaka dola
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira amesema kwamba kazi ya chama hicho kwa sasa ni kuisaka dola kwani mchakato wa kura za maoni zilishapita hivyo hakuna sababu ya kuwa na mgawanyiko tena.