Jeshi la Polisi Tanzania laonya na kupiga marufuku maandamano ya CHADEMA
Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limetoa onyo kali na kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa na viongozi wa CHADEMA yatakayofanyika tarehe 23 Septemba 2024. Polisi wameonya kwamba mtu yeyote atakayepatikana akiingia barabarani atakabiliwa na hatua kali za kisheria.