Gambia yatangaza mlipuko wa ugonjwa wa mpox
Gambia imeripoti mlipuko wa ugonjwa wa mpox siku ya Jumanne baada ya kugunduliwa kwa kisa kimoja kupitia mfumo wa kawaida wa ufuatiliaji wa magonjwa, huku nchi kadhaa jirani zikiripoti ongezeko la maambukizi hivi karibuni.