Asilimia 34.3 ya Vijana Wanapata VVU kila Mwaka
Haya yameelezwa leo Aprili 9,2025, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambapo ameeleza kuwa takwimu zilizopo watu 1,690,948 wanaishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU).