SADC yatangaza mshikamano na DRC
Mkutano huo ulifanyika baada ya wanajeshi 16 kutoka Afrika Kusini na Malawi, pia wanachama wa SADC, kuuawa katika mapigano ya karibuni karibu na Goma, ambako walikuwa wamepelekwa kama sehemu ya juhudi za kudumisha amani.