Safu mpya ya uongozi wa ACT Wazalendo ilivyoweka kipaumbele cha uchaguzi ili kushika dola.
Wiki hii ilikuwa ni wiki ya hekaheka za vikao vya kamati kuu vya chama cha upinzani cha ACT Wazalendo, ambayo imeishia katika mkutano mkuu wa chama hicho ambao ulitambulisha safu ya viongozi wapya ikiwa ni sehehmu ya kupokezana kijiti kama ambavyo Katiba yao inawataka kufanya hivyo kila inapofika miaka mitano.