Mwanafunzi ajinyonga kisa kutoipenda shule aliyokuwa akisoma
Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Lumbira kata ya Luanda wilayani Mbozi mkoani Songwe,Japhari Mwashitete (16) amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga darasani huku kukiwa na ujumbe wa sababu ya kujinyonga ukieleza kuikataa shule hiyo.