Amnesty International :Polisi walitumia nguvu zaidi kuwaondoa wamaasai Loliondo
Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International imeituhumu mamlaka nchini Tanzania kwa kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na kuwazuilia jamii ya wamaasai wakati wakiwatimua katika eneo la Loliondo.