Tanzania yaitaka Jumuiya ya Kimataifa kusaidia mchakato wa kuwarudisha wakimbizi wa Burundi nchini kwao
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi nchini Tanzania, Mhandisi Hamad Masauni amezitaka Jumuiya ya Kimataifa na Washirika wa Maendeleo kusaidia mchakato wa kuwarudisha Wakimbizi wa Burundi kwa hiari nchini kwao kwa kuweka sawa mazingira ya ndani ya nchi hiyo.