Urusi yaandikisha maelfu kutoka Syria kujiunga na vita Ukraine
Kremlin ilisema wiki iliyopita kwamba watu wa kujitolea, wakiwemo kutoka Syria, wanakaribishwa kupigana pamoja na jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Kremlin ilisema wiki iliyopita kwamba watu wa kujitolea, wakiwemo kutoka Syria, wanakaribishwa kupigana pamoja na jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Msururu wa milipuko mikali ilitikisa maeneo ya makazi ya watu wa Kyiv mapema Jumanne na kuua watu wawili, saa chache kabla ya mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi kutarajiwa kuanza tena.
Uamuzi wa serikali ya Uingereza kufungia mali yake unalemaza shughuli za Klabu ya Soka ya Chelsea, kiungo muhimu cha utajiri wa Abramovich, na kutoa pigo lingine kubwa kwa biashara yake.
Takriban watoto 71 wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa nchini Ukraine tangu Rais wa Urusi Vladimir Putin kuanzisha vita Februari 24, afisa wa bunge la Ukraine alisema Alhamisi.
Umoja wa Mataifa unasema watu milioni 1.7 wameikimbia Ukraine, na kuufanya mzozo huu kuwa mkubwa zaidi na unaokuwa kwa kasi zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia.
Vladamir Putin ameahidi atatimiza lengo lake kwa njia yoyote ile iwe “kwa mazungumzo au kupitia vita”
Urusi ni mojawapo ya nchi zinazozalisha mafuta ghafi kwa wingi zaidi duniani na pia inaongoza kwa kusambaza gesi asilia.
Maandamano ya kupinga vita nchini Urusi yameendelea licha ya onyo kutoka kwa mamlaka na hatari ya kufungwa jela.
Beijing imejipata katika hali ngumu ya kidiplomasia katika kipindi chote cha mzozo huo, ikikataa kulaani mshirika wake wa karibu Moscow.
Zelensky alitoa wito wa mazungumzo ya moja kwa moja na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin, akisema “ndio njia pekee ya kukomesha vita hivi”.