Search
Close this search box.
Europe

Watu 7 Wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kanisani Ujerumani

11

Watu zaidi ya 7 wameripotiwa kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye jumba la mikutano la Jehovah Witness katika jiji la Hamburg kaskazini mwa Ujerumani.

Polisi wanasema kuwa mtu aliyepiga risasi alikuwa pekee na anadhaniwa amekufa. Haijabainika iwapo mshambuliaji huyo ni miongoni mwa vifo  saba vilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya Ujerumani.

Watu kadhaa pia walijeruhiwa katika ufyatulianaji wa risasi kwenye mtaa wa Deelböge katika wilaya ya Gross Borstel ya jiji hilo.

Polisi wanasema walimpata mtu aliyekufa katika eneo la tukio ambaye wanaamini kuwa huenda alikuwa mhusika na uchunguzi unaendelea.

Maafisa wanasema vile vile  walisikia mlio wa risasi kutoka sehemu ya juu ya jengo hilo na wakapanda juu, ambapo pia walimkuta mtu mmoja hadi sasa hawana  hakukuwa na dalili zozote kwamba wahalifu wowote walitoroka.

polisi bado hawajawatambua wahasiriwa na uchunguzi katika eneo la uhalifu inaendelea.

Comments are closed

Related Posts