KUZUKA UPYA KWA UGONJWA WA VIRUSI WA MARBURG

Ugonjwa wa Marburg ulizuka mara ya kwanza nchi Ujerumani katika miji ya Marburg na Frankfurt.

0

Ugonjwa wa Marburg ulizuka mara ya kwanza nchi Ujerumani katika miji ya Marburg na Frankfurt.

Tangu ugonjwa huo ulipogunduliwa mwaka 1967 takriban watu 478 wamefariki. Ugonjwa wa Virusi wa Maburg umezuka upya nchini Guinea magharibi mwa Afrika.

Maafisa wa afya nchini humo wanafuatilia watu 72 waliokuja karibu na mgonjwa aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.Kisa cha hivi maajuzi kiliripotiwa 9 Agosti na mtu huyo alifariki.Waziri wa afya nchini Guinea, Remy Lamah,amesema kisa hicho cha Marburg kilizuka katika eneo la kusini mwa Gueckedou.

Waziri Lamah, akiwasiliana na Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema, wameweka mikakati madhubuti ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na kuhamasisha ummakuhusu ugonjwa huo.Hakuna dawa au chanjo dhidi ya Ugonjwa wa Virusi wa Marburg.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted