Kumbukumbu ya Tundu Lissu miaka minne baada ya kushambuliwa kwake

“Kila wingu jeusi linautepe mweupe, nasheherekea maisha mapya.” Tundu Lissu

0

Mhe. Tundu Lissu, Naibu Mwenyekiti CHADEMA

Kila wingu jeusi linautepe mweupe, nasheherekea maisha mapya” Tundu Lissu

Makamu mwenyekiti wa chama kikuu pinzani nchini Tanzania, Mhe. Tundu Lissu ni mwanasiasa wa miaka mingi. Kabla kujiunga na siasa alisomea uanasheria na baadae kujitosa katika siasa na kushinda kiti cha ubunge katika eneo bunge la Singida mashariki,ambapo alihudumu kama mbunge hadi mwaka 2010.

Tarehe 23 Agosti 2017, nyumba ya Mhe. Tundu Lissu ilioko maeneo ya Area D Dodoma ilivamiwa na polisi na kufanyiwa msako baada ya yeye kukamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa madai ya uchochezi na kumtusi Rais John Pombe Magufuli.

Mchana wa Septemba 7 2017, kulikuwa na jaribio la mauaji dhidi ya Tundu Lissu alipokuwa akitoka majengo ya bunge. Lissu alishambuliwa kwa risasi 16, hali yake ilikuwa hoi alipofikishwa uwanja wa ndege ili kusafirishwa kuenda jijini Nairobi na baadae nchini Ubelgiji alikofanyiwa upasuaji, kwa ujumla Mhe. Lissu amefanyiwa upasuaji mara 25 kuondoa risasi zilizochana mwili wake.

Mhe.Tundu Lissu, Naibu Mwenyekiti CHADEMA

Mwaka wa 2020 alirudi Tanzania kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa mwaka huo,Rais Magufuli wa chama tawala cha CCM alishinda uchaguzi huo kwa muhula wa pili.

Mhe.Tundu Lissu na viongozi wengine wa chama cha CHADEMA pamoja na asasi za kiraia na wanasiasa wengine nchini Tanzania wamekuwa wakiendeleza msukumo wa kupatikana kwa katiba mpya. Kumeandalia makongamano tofauti nchini humo ambayo yamesababisha kukamatwa kwa baadhi ya viongozi wa chama kikuu pinzani nchini Tanzania, CHADEMA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA walikamatwa mjini Mwanza baada ya kongamano la kudai katiba mpya na wamekuwa kuzuizini kwa zaidi ya siku 40.

Mhe. Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA

Katika mahojiano, Mhe. Tundu Lissu alisema

“Kuna wanachama wetu zaidi ya 400 wamekamtwa sehemu mbalimbali, tangu mwenyekiti
wetu alipokamatwa, kuna wengine wamekamatiwa mpaka kanisani wakiwa wanasali baada
ya kuomba misa kanisa katoliki Mwanza.Wamekamatiwa ndani ya kanisa, Askofu wa
kanisa Katoliki Mwanza amesema hawa watu niliwaalika kuja kufanya misa, na
wameshtakiwa eti kwa vurugu kanisani.Tumerudi kwenye siasa za Magufuli”- Tundu Lissu,
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA”

Mhe, Tundu Lissu anasema, hatachoka kudai katiba mpya kwani itawafaa watanzania wote kwa ujumla, na hata kama alijeruhiwa vibaya miaka minne iliyopita mapambano bado yanaendelea, ilimradi yupo hai, anasheherekea maisha mapya.

“Tanzania ni nchi niipendayo na nitaendelea kuipigania” Mhe. Tundu Lissu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted