Wanafunzi wa Uganda wadaganya kuwa wazazi wameaga dunia ili wapate mikopo ya elimu

Wanafunzi wa Uganda wadaganya kuwa wazazi wameaga dunia ili wapate mikopo ya elimu

0

Serikali ya Uganda imefutilia mbali mikopo ya wanafunzi 47 wa vyuo vikuu ambao walidanganya juu ya vifo vya wazazi wao ili kufaidika na mpango wa mikopo ya wanafunzi. Mamlaka inayosimamia mikopo ya wanafunzi imewaamuru wanafunzi waliofutiwa mikopo kurudisha pesa walizopewa baadaya ripoti nyingine kuonyesha kuwa wanafunzi wengine walidanganya kuwa walikuwa na ulemavu na wengine ambao
walighushi nyaraka za kuomba mikopo.

Wanafunzi hao 47 walikuwa kati ya wanafunzi 1,113 waliofaidika na mkopo wa elimu wa mwaka 2020/2021. Vyanzo vinasema wanafunzi walioathirika walidanganya kuwa
wazazi wao wameaga dunia ilhali wazazi wao walikuwa hai.

Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu (HESFB) huwapa kipaumbele wanafunzi wenye ulemavu,mayatima,wanafunzi wa kike na wanafunzi kutoka kaskazini mwa Uganda.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted