Je, kama mzazi upo tayari mwanao ajiunge na mtandao mpya wa Instagram kids?

Mipango yakuanzisha mtandao wa Instagram hususan kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 13 kwa jina Instagram Kids umesitishwa kwa sasa.

0

Mipango yakuanzisha mtandao wa Instagram hususan kwa watoto waliochini ya umri wa miaka 13 kwa jina Instagram Kids umesitishwa kwa sasa.

Facebook, kampuni inayomiliki Instagram, imesema itachukua muda kusikiliza maoni ya wazazi, waalamu, watunga sera na wasimamizi, amesema mkuu wa Instagram Adam Mosseri.

Hii inafuatia utafiti uliotolewa na jarida la Wall Street Journal kuwa Instagram inawaathiri vibaya vijana hususan wasichana. Ila katika taarifa yake, mtafiti mkuu wa Facebook, Pratiti Raychoudhury, anasema madai hayo si ya ukweli.

Instagram kwa sasa inahitaji mtu awe na umri wa zaidi ya miaka 13 ili kutumia mtandao huo, ila kuna watoto chini ya umri wa miaka 13 ambao wanatumia mtandao huo kwa sasa.Kampuni hiyo pia imesema kuwa, kuwepo kwa mtandao mahsusi kwa watoto yaani Instagram Kids,itakuwa suluhu kwa watoto wanaojiunga na Instagram kwa kudaganya umri wao, na kuwa App hiyo mpya itawasaidia watoto kuwasiliana na jamaa zao.

Mnamo mwezi wa Aprili, barua kutoka Kampeini ya “Campaign for a Commercial-free Childhood” iliyotiwa saini na makundi na watu 99, ilidai kuwa mtandao huo unaopigia debe “muonekano wa mtu”ulikuwa hatari kwa afya ya kiakili ya watoto na usalama wa watoto, na kutaka mpango mzima wa Instagram Kids kufutiliwa mbali.

Bwana Mosseri anaamini ni bora kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 10 – 12 kuwa na mtandao wao ambapo utakuwa rahisi kuthibitisha umri wa mtoto kabla hajaruhusiwa kujiunga na mtandao huo.

Adam Mosseri, Msimamizi Mkuu wa Instagram

Ukweli ni kwamba watoto tayari wako mtandaoni” alisema Adam Mosseri.

Wakati mradi ukiwa umesitishwa kwa sasa, Instagram inaimarisha njia za kudhibiti wale wanaojiunga na Instagram ikilenga watoto walio kati ya umri wa miaka 13- 19.

Tovuti ya habari za teknolojia, The Verge imesema kuwa majibu ya Facebook, “yamepuuza masuala mengi yaliyoibuliwa ikiwemo ripoti ya WSJ,pamoja na madai kuwa vijana wengi wanahisi maisha yao yameingiana sana na mtandao wa Instagram.”

Mkuu wa usalama wa kimataifa wa Facebook, Antigone Davis atakwenda mbele ya kamati ya seneti ya Marekani kujibu maswali, ambapo anatarajiwa kuulizwa kuhusu ripoti ya Wall Street Journal na mipango ya Instagram Kids.

Mnamo mwezi Mei wanasheria kutoka majimbo 44 nchini Marekani waliihimza Facebook kuachana na mipango ya Instagram kwa watoto, wakisema watoto hawana uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii bila kuwepo madhara, wakiongeza kuwa kuna njia bora za wao kuwasiliana na familia na jamaa zao.

Bwana Mosseri na Katibu Mkuu Mtendaji wa Facebook Mark Zuckerberg wamesema mitandao ya kijamii inaweza kuwasaidia watoto kukuza uhusiano na jamaa na marafiki.

Mark Zuckerberg, Katibu Mkuu Mtendaji wa Facebook
In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted