Vifo kutokana na virusi vya corona vyapungua.

Shirika la Afya Duniani, (WHO) limesema idadi ya vifo vya kila wiki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imeendelea kpuungua na hivi sasa imefikia kiwango cha chini zaidi kwa...

0

Shirika la Afya Duniani, (WHO) limesema idadi ya vifo vya kila wiki kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imeendelea kpuungua na hivi sasa imefikia kiwango cha chini zaidi kwa takribani mwaka mmoja.

WHO imesema kitakwimu ikilinganishwa na awali idadi hiyo ya vifo 50,000 kila wiki ni ndogo lakini kiuhalisia bado ni kubwa kwa kutambua kuwa bado watu wanafariki dunia.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva,Uswisi amesema idadi ya vifo vya COVID-19 inapungua kila ukanda wa dunia isipokuwa barani Ulaya ambako nchi kadhaa zinakumbwa na wimbi jipya la wagonjwa na vifo.

“Na bila shaka, idadi kubwa ya vifo ni kubwa miongoni mwa nchi na watu ambako bado chanjo siyo rahisi kupatikana.Kama unavyofahau nchi 56 ambazo zilikuwa zimeenguliwa kutoka soko la chanjo za COVID-19 duniani hazikuweza kufikia lengo la kuchanja asilimia 10 ya wananchi wake hadi mwisho wa mwezi uliopita wa Septemba na nyingi ziko Afrika.” amesema Dkt. Tedros.

Hata hivyo amesema nchi nyingi zaidi ziko hatarini kushindwa kufikia lengo la kuchanja asilimia 40 ya wananchi wake ifikapo mwishoni mwa mwaka huu akitaja nchi kama vile Burundi, Eritrea na Korea Kaskazini ambazo hazijaanza kutoa chanjo dhidi ya Corona.

Mataifa mengine hayana chanjo za kutosha, licha ya kwamba yameanzisha kampeni za chanjo kufikia lengo.

Na kwa mantiki hiyo amesihi nchi na kampuni zinazodhibiti usambazaji wa chanjo duniani kupatia kipaumbele jukwaa la kimataifa la kusaka na kugawa chanjo duniani, COVAX na mpango wa Afrika wa kusaka chanjo hizo, AVAT.

Amegusia pia nchi zenye mizozo na ghasia ambako ufikishaji chanjo una mkwamo akisema WHO na wadau wake wanafanya kazi na mataifa hayo ili kuimairisha uwezo wa kiufundi na kivifaa ili chanjo ziweze kusambazwa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted