Sabaya akutwa na kesi ya kujibu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu Sabaya na wenzake sita katika kesi inayowakabili ya Uhujumu Uchumi

0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imewakuta na kesi ya kujibu watuhumiwa saba wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, ambaye anasikiliza kesi hiyo namba 27 ya mwaka 2021, amesema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi 13 wa Jamhuri na vielelezo 12, mahakama imeona washitakiwa wote saba wana kesi ya kujibu.

Baada ya uamuzi huo mdogo, Wakili wa utetezi Mosses Mahuna ameieleza mahakama kuwa watakuwa na mashahidi wasiozidi 10 na vielelezo ambavyo hajajua idadi yake na kuomba mahakama iwape muda waweze kujipanga kwa ajili ya kuanza kujitetea.

Ombi hilo la wakili wa utetezi Mosses limekubaliwa na Mahakama hiyo hivyo Hakimu Kisinda ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 17 mwaka huu ambapo watuhumIwa hao wataanza kujitetea.

Katika kesi hii Washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano la kwanza wanadaiwa kuwa mnamo Januari 22, 2021 wliongoza genge la uhalifu na kosa la tano ambalo ni utakatishaji fedha linawakabili washitakiwa wote saba  wanadaiwa kupata shilingi milioni 90 kutoka kwa mfanyabiashara Francis Mrosso, huku wakijua kupokea fedha hizo ni zao la kosa la vitendo vya rushwa.

Kosa la pili, tatu na nne Sabaya peke yake ameshitakiwa kwa makosa ya kujihusisha na rushwa ambapo anadaiwa kuchukua shilingi milioni 90 na matumizi mabaya ya ofisi akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro.

Mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted