Mifumo ya elimu yatakiwa kwenda sawa na kasi ya Teknolojia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema mifumo iliyopo sasa imepitwa na wakati

0

Ikiwa leo ni siku ya elimu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la COVID-19 na changamoto nyingine zinazokabili Dunia hivi sasa zimedhihirisha umuhimu wa kurekebisha mfumo wa elimu ili uweze kukidhi mahitaji ya sasa.

Hivi sasa dunia inakua kwa kasi kutokana na mifumo ya teknolojia na mambo mengi yanafanywa katika mifumo hiyo Guterre amesema “dunia yetu inabadilika kwa kasi ya haraka mno, ubunifu katika teknolojia, mabadiliko yasiyo ya kawaida kwenye dunia ya ajira, dharura ya mabadiliko ya tabianchi na kuenea kwa ukosefu wa imani baina ya watu na taasisi.”

Na zaidi ya yote, mifumo ya kawaida ya elimu inahaha kutoa elimu, stadi na maadili ambayo ni lazima kuijenga ili kuwepo na mustakabali bora, salama na unaojali mazingira kwa wote.

Akitolea  mfano wa janga la COVID-19 amesema janga hili limetibua sekta ya elimu duniani kote kwani takribani wanafunzi bilioni 1.6 wa Vyuo Vikuu na shule masomo yao yalivurugika janga tu la Corona lilipoanza na hadi sasa bado halijaisha.

Guterres anaonya “tusipochukua hatua, idadi ya watoto wanaoacha shule katika nchi zinazoendelea na ambao hawajui kusoma na kuandika inaweza kuongezeka kutoka asilimia 53 hadi asilimia 70.”

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu amesema kuwa sekta ya elimu ni zaidi ya hoja ya kuipata na ukosefu wa usawa kwa kuwa “elimu ni bidhaa ya umma na ni jambo muhimu linalohitajika kufanikisha ajenda nzima ya 2030 kwa maendeleo endelevu. Jamii ya kimataifa haiwezi kukubali kutokuwa na uhakika katika utoaji wa elimu, tena bora na inayoendana na wakati.”

Ameongeza kuwa  kwa kutambua hilo ndio maana ataitisha mkutano wa viongozi wa kurekebisha mfumo wa elimu. “Muda umefika kuchochea upya azma yetu ya pamoja kwa elimu. Hii ina maana kuwekeza katika mipango thabiti ya kusaidia wanafunzi kupata mafunzo ambayo walipoteza.”

Amefafanua kuwa mkutano wa viongozi wa kufanyia marekebisho ya elimu utakuwa ni wa mara ya kwanza kwa viongozi wa dunia, vijana na wadau wote wa elimu wanakutana pamoja na kuzingatia masuala hayo ya msingi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted