Uwekezaji waongezeka Tanzania

Sababu yatajwa kuwa ni kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji nchini

0
Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema kwa sasa kiwango cha uwekezaji, thamani na kiasi cha ajira katika miradi inayoanzishwa vimeongezeka hatua ambayo imetajwa kuwa ni tija kwa Taifa.

Msigwa amesema serikali imekuwa ikiboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa kusikiliza changamoto za wawekezaji na kuzipatia ufumbuzi ikiwa ni pamoja na kuondoa urasimu, na kurahisisha utoaji wa vibali muhimu na hatua hizo zimechangia wawekezaji wengi kujenga imani na kuwekeza hapa nchini.

Ameongeza kuwa mwaka jana miradi 222 ilisajiliwa katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) yenye thamani ya shilingi trilioni 6.1 wakati kipindi kama hicho mwaka 2020 miradi iliyosajiliwa ilikuwa 173 yenye thamani ya shilingi trilioni 2.1

Miradi hiyo iliyosajiliwa mwaka jana ilizalisha ajira zaidi ya 49,944 wakati miradi ya mwaka 2020 ilizalisha ajira 14,819, ambapo miradi iliyosajiliwa mwaka jana 66 ni ya wazawa na 60 ni ya ubia.

Kuhusu mkongo wa taifa, Msigwa amesema mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi  bilioni 600 na unatarajiwa kutekelezwa kwa umbali wa kilomita 15,000 na hadi sasa mkongo huo umefika kilometa 8,119.

Amesema hivi sasa utekelezaji mwingine wa kilomita 4,442 unaendelea huku pia maboresho ya uwezo wa mkongo yakifanywa kutoka uwezo wa G 2 hadi G8.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted