Rais Samia kufanya ziara nchini Ufaransa na Ubelgiji

Akiwa huko anataraja kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

0
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais Samia Suluhu Hassan anatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini Ufaransa na baadae kwenda Ubelgiji kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Taarifa iliyotumwa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus, imeeleza kuwa, Rais Samia anatarjia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaojadili kuhusu Rasilimali Bahari Duniani.

Katika ziara hiyo pia Samia atashuhudia utiaji saini baina ya Serikali ya Tanzania na Ufaransa katika sekta za miradi  ya maendeleo, ushirikiano katika masuala ya uchumi wa buluu, usalama wa bahari, sekta ya usafri na maendeleo endelevu.

Aidha taarifa imeeleza kuwa pamoja na masuala mengine, Rais Samia Suluhu anatarajiwa kuzungumza na Watanzania waishio nchini Ufaransa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted