Mwanaume wa miaka 40 apandikizwa uume 

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika Mashariki na ya Kati .

0

Hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan imesema imefanikisha upandikizaji wa kwanza wa uume katika kanda ya Afrika Mashariki na ya Kati .

Upasuaji huo maalum amefanyiwa mwanamume wa umri wa miaka ya 40 ambaye alikuwa na Hali ya maumbile nyeti kushindwa kuwa tayari, ambayo kwa kitaalamu inajulikana kama Erectile dysfunction (ED), tatizo ambalo limemsumbua kwa miaka kadhaa kulingana na taarifa ya hospitali hiyo .

Tatizo hilo hutokea wakati ambapo mwanamume hawezi kushiriki katika tendo la ndoa kwa dakika 15 mfululizo na mgonjwa huyo alikuwa amepokea aina nyingine za matibabu bila hali yake kuboreka .

‘Upandikazaji huu huchukua takriban saa moja na na unahusisha kuweka kifaa maalum(Prosthesis) ambacho kinapachikwa kwenye uume na kumwezesha mtu kufanya tendo la ndoa wakati wowowte bila kuhitajika kutumia dawa nyingine’ amesema Dkt.Ahmed Yousef aliyeiongoza upasuaji huo .

Upasuaji huo umefanyika kwa mara ya kwanza katika kanda hii kwa sababu unahitaji utaalumu wa kipekee na ufahamu wa kitengo cha tiba ya Urolojia.

Inakadiriwa kuwa asilimia 15-20 ya wanaume wana matatizo ya Erectile dysfunction (ED) na mshindo wa mapema (Premature Ejaculation) na wengi wanaoteseka hukaa kimya kwa sababu ya hali hizo .

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted