GGM kuilipa TANESCO bilioni 5 kila mwezi

Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesaini mkataba wa kuuzia umeme Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) ambao utawezesha shirika hilo kupata shilingi bilioni 5 kwa mwezi.

0

Shirika la Umeme nchini (Tanesco) limesaini mkataba wa kuuzia umeme Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) ambao utawezesha shirika hilo kupata shilingi bilioni 5 kwa mwezi.

Kwa sasa mgodi huo unatumia nishati ya mafuta ambayo kwa mwezi unalazimika kununua mafuta ya kuendeshea mitambo kwa gharama ya dola za kimarekani million tatu kwa mwezi.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Maharage Chande amesema mradi huo ukikamilika utondoa gharama kubwa ya wanayoingia GGM ya kununua mafuta.

Amesema kupatikana kwa umeme pia kutasaidia mgodi huo kutunza mazingira na kuondokana na hewa ukaa wanaozalisha sasa.

Makamu wa Rais wa GGM nchini Tanzania na Ghana, Saimon Shayo amesema kwa miaka 20 wamekuwa wakitumia umeme wa kuzalisha kwa mafuta.

Amesema kwa sasa shirika la Tanesco linajenga njia ya KV 33 kwenda mgodini na mgodi utakuwa unajenga kituo cha kupoozea umeme ambavyo vyote vinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka huu.

Shayo amesema pamoja na kuwa mafuta wanayotumia yanamsamaha wa kodi lakini bado gharama ya uzalishaji umeme ni kubwa kuliko umeme unaotolewa na Tanesco.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted