Mtandao wa Instagram wafungiwa Urusi

Watumiaji wa mtandao wa Instagram nchini Urusi wamepewa taarifa kuwa huduma hiyo imesitishwa kuanzia saa sita usiku Jumapili ya March 14, 2022

0

Watumiaji wa mtandao wa Instagram nchini Urusi wamepewa taarifa kuwa huduma hiyo imesitishwa kuanzia saa sita usiku Jumapili ya March 14, 2022 baada ya Mmiliki wake Meta Platforms kutangaza wiki iliyopita kuwa itawaruhusu Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Ukraine kutuma ujumbe wa kushinikiza Wavamizi wakirusi wauawe.

Emails kutoka kwa Mdhibiti wa Mawasiliano wa Serikali ya Urusi iliwataka Watumiaji kuhamisha picha na video zao kutoka kwenye mtandao huo wa Instagram kabla ya kuzimwa ikiwa ni siku 2 baada ya Kampuni ya Meta ambayo pia inamiliki mtandao wa Facebook (FB) kusema mabadiliko ya muda mfupi katika sera yake ya matamshi ya chuki yanahusu Ukraine pekee kufuatia uvamizi wa Urusi wa Februari 24.

Kampuni hiyo ilisema itakuwa vibaya kuwazuia Waukraine kuonyesha hisia zao na hasira kwa vikosi vya kijeshi vinavyoivamia, kauli ambayo ilipokelewa kwa hasira na Serikali ya Urusi na kuifanya kufungua uchunguzi wa jinai dhidi ya Kampuni ya Meta.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted