Ndege iliyobeba watu 133 yaanguka China

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamalaka ya Usafiri wa Anga ya China, ndege hiyo aina ya Boeing-737 ilikuwa ikitokea mji wa Kunming kuelekea Guangzhou.

0

Ndege ya Shirika la Ndege la China iliyokuwa imebeba watu 133 imeanguka kwenye milima kusini mwa Guangxi nchini China.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mamalaka ya Usafiri wa Anga ya China, ndege hiyo aina ya Boeing-737 ilikuwa ikitokea mji wa Kunming kuelekea Guangzhou.

Hata hivyo ndege hiyo ilipopoteza mawasiliano kwenye mji wa Wuzhou.

Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria 123 pamoja na wahudumu 10.

Tayari timu ya uokoaji imetumwa kwenye eneo ambako ndege hiyo imepata ajali.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted