Takriban Wakenya 250,000 waliofariki wapatikana katika sajili ya bodi ya uchaguzi

Takriban wapiga kura nusu milioni zaidi walipatikana kuwa wamejisajili mara mbili na zaidi ya watu 226,000 walisajiliwa kwa kutumia stakabadhi ambazo si zao.

0
Wafula Chebukati, Mwenyekiti Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) ilitangaza Jumatano kwamba wapigakura 246,465 waliofariki walipatikana kwenye sajili yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 2022.

Hili lilikuwa miongoni mwa makosa kadhaa ambayo Tume iligundua, na kuilazimu kuahirisha uchapishaji wa rejista ya wapiga kura Jumatano.

Takriban wapiga kura nusu milioni zaidi walipatikana kuwa wamejisajili mara mbili na zaidi ya watu 226,000 walisajiliwa kwa kutumia stakabadhi ambazo si zao.

Wengine walikuwa wamejiandikisha na hati batili, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilisema kwenye taarifa kuhusu hitilafu zinazoathiri zaidi ya watu milioni moja.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa kwa sababu kutokana na matokeo hayo tume itachelewa kuidhinisha sajili ya mwisho ili kuchapishwa kabla tarehe 20 Juni.

Makosa ya uchaguzi katika chaguzi zilizopita nchini Kenya yamesababisha vurugu na maafa.

Uchaguzi wa mwaka huu utafanyika tarehe 9 Agosti.

Kufikia sasa, IEBC imewaidhinisha wagombeaji wanne kuwania kiti cha urais — Raila Odinga kutoka muungano wa Kisiasa Azimio la Umoja, William Ruto wa United Democratic Alliance-UDA, George Wajackoyah kutoka Roots Party na David Mwaure Waihiga wa Agano Party.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted