Jackline Chepkoech ashindia Kenya dhahabu katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi

Jackline Chepkoech mwenye umri wa miaka 18 ajishindia dhahabu katika mbio za mita 3000 za SteepleChase katika rekodi mpya ya dunia ya 9:15.68. Alishinda medali ya pili ya...

0

Jackline Chepkoech mwenye umri wa miaka 18 ajishindia dhahabu katika mbio za mita 3000 za SteepleChase katika rekodi mpya ya dunia ya 9:15.68. Alishinda medali ya pili ya dhahabu kwa Kenya kwenye Michezo ya Commonwealth.

Mwanariadha huyo chipukizi alinyakua taji hilo mbele ya Elizabeth Bird wa Uingereza aliyeingia katika nafasi ya pili kwa dakika 9:17.79 na Mwanariadha wa Olympia wa Uganda Peruth Chemutai aliyeibuka wa tatu kwa saa 9:23.24 siku ya Ijumaa katika uwanja wa Alexander Stadium, Birmingham.

“Nilikuwa na uhakika wa ushindi. Mpango wangu ulikuwa ni kuondoka na mizunguko miwili kwenda kumpiga Chemutai. Hangenipiga hata bila kuanguka lakini ninamsikitikia.” Alisema Chepkoech.

Alijitolea ushindi wake kwa wazazi wake Wilson Chepkes na mamake Juliana nyumbani kwao Olenguruone, kaunti ya Nakuru. “Wamenipa usaidizi wote na wakati wa kufanya mazoezi na hiyo ilinipa amani ya akili ya kuzingatia mafunzo.”

“Zaidi ya yote nisingefanikisha haya bila Mungu, ninamshukuru kwa neema yake na afya njema.” Chepkoech alisema zaidi. Pia alimpongeza Faith Cherotich wa Kenya ambaye alishinda mbio za Dunia za Under-20 3000m kuruka viunzi huko Cali, Colombia.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted