UN yaipongeza Kenya kwa kushiriki Uchaguzi Mkuu kwa amani

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric kutoka New York nchini Marekani imesema, Katibu Mkuu anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja na mashirika...

0

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wananchi wa kenya kwa kupiga kura kwa amani wakati wa Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Agosti 9, 2022

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu Stéphane Dujarric kutoka New York nchini Marekani imesema, Katibu Mkuu anatambua kazi muhimu iliyofanywa na mamlaka ya Kenya pamoja na mashirika mengi yote yanayohusika na usimamizi wa uchaguzi, ushirikishwaji wa wadau mbalimbali wa kitaifa na dhamira ya dhati isiyoyumbishwa ya wapiga kura kutekeleza haki yao ya kikatiba ya kupiga kura. 

“Katibu Mkuu ana imani wadau wote wa kisisasa na wananchi wa Kenya wataendelea kuonesha kiwango hicho hicho cha utulivu, Subira na heshima kwa mchakato huo wa uchaguzi wakati huu wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya kura kwa mujibu wa muda uliowekwa kisheria” amesema Dujarric 

Katibu Mkuu amesisitiza uwepo wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkonoi juhudi zote zinazofanyw ana mamlaka ya nchi hiyo na wananchi wote wa Kenya ili kuhakikisha wanaendeleza mchakato wa kidemokrasia nchini humo. 

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted