Ubalozi wa Marekani Kenya wawatahadharisha tena raia wake

Ubalozi wa Marekani watoa ilani ya usalama kwa raia wake nchini Kenya.

0

Ubalozi wa nchi ya Marekani nchini Kenya sasa inawataka raia wake kuchukua tahadhari kubwa wakati ambapo mahakama ya upeo inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu uchaguzi wa urais mnamo tarehe 5 Septemba 2022.

Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari, Ubalozi huo unasema taifa la Kenya limekuwa likikumbwa na ghasia za baada ya uchaguzi katika kila chaguzi tangu mwaka wa 2008.

Taarifa hiyo imewataka maafisa wake wanaoishi mjini Kisumu kuwa waangalifu wakati ambapo uamuzi kuhusu matokeo ya uchaguzi uliofanyika agosti tisa unatarajiwa kubainikakuambatana na mahakama ya juu.

 ‘’Uchaguzi unaohusishwa na maandamano na mikutano mara kwa mara hutokea baada ya uchaguzi, na mara nyengine husababisha trafiki barabarani kutokana na maandamano ambayo hushirikisha ghasia hali ambayo uhitaji maafisa wa polisi kuingilia kati’’, ilisema Taarifa hiyo.

Kisumu ni mji wa nyumbani wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia chama cha Orange Democratic Movement ilioko ndani ya muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga ambaye aliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo yaliotolewa na tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC kumfanya William Ruto kama mshindi wa urais.

Siku ya Jumanne balozi wa Marekani Kenya Margaret Whitman alimpa kongole Odinga kwa kuwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo hayo ya urais.

Balozi wa Marekani Kenya Meg Whitman na gavana wa kaunti ya Kisumu Anyang’ Nyong’o

Whitman aliyezungumza alipozuru mji wa Kisumu alisema ameridhishwa na jinsi amani ilivyodumishwa na wakenya katika kipinci hiki cha uchaguzi na kuwataka wadau mbalimbali kuwa na subra wanapoendelea kusibiri uamuzi kutolewa na majaji saba wa mahakama hiyo.

Hata hivyo, balozi huyo alisema kuwa ilani  ya usalama iliyotolewa na ubalozi Marekani mapema mwezi agosti kuhusu kuzuru kaunti ya Kisumu ilikuwa inalenga kuwahakikishia raia wa Marekani wanaoishi Kisumu wako salama na haikutolewa kuonyesha taswira mbaya kuhusu kaunti ya Kisumu.

Zoezi la kusikiza upande zote katika kesi hiyo ya urais ilianza siku ya jumanne na inakamilika leo ijumaa kabla ya majaji hao saba kukongamana kwa siku mbili ili kuandaa uamuzi wao.

Siku ya jumatatu tarehe 5 septemba mahakama hiyo ya upeo chini ya uongozi wa jaji mkuu Martha Koome itatoa uamuzi wake kuhusu kesi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa katika mustakabali wa Kenya.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted