Omanyala Ni Moto Wa Kuotea Mbali,Atisha Ufaransa

Ferdinand Omanyala alishamiri katika mashindano ya mbio za ukumbini nchini Ufaransa kwa kutwaa ushindi wake wa pili usiku wa Jumamosi.

0


Mshikilizi wa rekodi ya mbio za mita 100 barani Afrika Ferdinand Omanyala alishamiri katika mashindano ya mbio za ukumbini nchini Ufaransa kwa kutwaa ushindi wake wa pili usiku wa Jumamosi.

bingwa huyo wa Jumuiya ya madola aliweka muda wa sekunde 6.57 akiwaonyesha kivumbi wapinzani wake akiwemo Arthur Cisse ambaye alimaliza katika nafasi ya pili ndani ya muda wa sekunde 6.57.

“Ni matokeo makubwa zaidi kwangu na nimefurahia sana.muda ni wa kasi zaidi na napania kuboresha zaidi katika mbio zijazo.Hii inaonyesha kuwa msimu wangu umeanza vizuri,” Omanyala alisema .

Omanyala alitamba kiurahisi katika pambano la mbio za mchujo akiibuka mshindi ndani ya muda wa sekunde 6.611.

Omanyala sasa atajiandaa kwa mbio zake za mwisho nchini Ufaransa,akisafiri Lievin ambako anatarajiwa kutimuka Jumatano.Baada ya hapo atapaa kurejea nyumbani Kenya na sasa kuwekeza dira yake katika mbio za shirikisho la riadha nchini Kenya AK ambako anatarajiwa kukimbia katika mkondo wa Nairobi Februari 24 mwaka huu.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted