Toeni Wasomi Zaidi Kama Magoha,Rais Mstaafu Kenya Uhuru Kenyatta Awaambia Wakaazi Gem.

Rais huyo mstaafu alisema kuwa watu wa eneo la Gem wanafaa kuwakuza maprofesa zaidi,wasomi na hata viongozi kama Magoha.

0

Aliyekwa rais Uhuru Kenyatta amewataka viongozi kuwacha ukabila na kuiga mfano wa aliyekuwa waziri wa elimu profesa George Magoha.


“Inafaa tuendeleza upendo kama wakenya,kama tu vile Profesa George Magoha alivyofanya,ukabila na chuki havikuhusishwa na Magoha,tuige kufuata nyayo zake,” alisema.


Rais huyo mstaafu pia alisema kuwa watu wa eneo la Gem wanafaa kuwakuza maprofesa zaidi,wasomi na hata viongozi kama Magoha.


“Tukuze wasomi zaidi kama Magoha nchini kenya” alisema Jumamosi katika mazishi ya Magoha.


Uhuru amesema kuwa Magoha alirejesha hadhi ya juu ya mitihani ya kitaifa wakati alipokuwa mwenyekiti wa baraza mitihani nchini Kenya (KNEC).


Amemshukuru marehemu profesa George Magoha kwa kurejesha uwazi katika mitihani ya kitaifa.


“Niliridhishwa zaidi ya kazi aliyofanya wakati akiwa naibu chansela wa chuo kikuu cha Nairobi” alisema.


Uhuru alidokeza kuwa kabla ya Magoha kuchukua usukani katika KNEC,taifa lilikuwa linashuhudua ongezeko la visa vya udanganyifu katika mitihani ya kitaifa.


“Wengi wenu mnakumbuka visa vya udanyifu wa mitihani nchini ambavyo vilikuwa sugu zaidi”alisema
Uhuru alikuwa ameandamana pamoja na kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga na baadhi ya mawaziri wa zamani waliohudumu katika serikali yake.


Viongozi wengine ambao walihudhuria mazishi ya Profesa George Magoha ni Waziri wa sasa wa elimu Ezekiel Machogu na katibu wa kudumu katika wizara ya elimu Belio Kipsang.


Magoha alifariki Januari 24 2023 akiwa na umri wa miaka 71.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted