Ni wasaliti hao,hawafai kuwa nasi! Viongozi wa ODM waliokutana na Rais Ruto matatani

Hatua ya baadhi ya viongozi kutoka chama cha ODM ambacho kipo katika mrengo wa upinzani nchini Kenya kukutana na Rais William Ruto imezidi kuzua joto la kisiasa,hii ikiwa...

0

Hatua ya baadhi ya viongozi kutoka chama cha ODM ambacho kipo katika mrengo wa upinzani nchini Kenya kukutana na Rais William Ruto imezidi kuzua joto la kisiasa,hii ikiwa baadhi ya masuala ambayo yalizungumziwa katika mkutano kisiasa wa mrengo wa Azimio-Oka ambao uliandaliwa kaunti ya Kisumu eneo la Nyanza Jumamosi.

Naibu kinara wa ODM Wycliffe Oparanya sasa anamtaka kinara wa chama hicho Raila Odinga kumpa idhini kupambana na viongozi hao wanaotajwa kuwa waasi.

Oparanya amedokeza kuwa kile ambacho viongozi hao walifanya ni kama hujuma kwa wapiga kura ambao waliwachagua kutumia tiketi ya chama cha ODM.

“Kama naibu kinatra wa ODM,nataka nipewe idhini kuwafurusha viongozi ambao walikwenda ikulu kukutana na Rais William Ruto bila idhini ya chama.,” Oparanya alisema.

Oparanya alidokeza kuwa wakati wa kipindi cha kusaka tiketi ya chama cha ODM viongozi hao ndio walikuwa msitari wa mbele kupiga kambi katika afisi ya kiongozi wa upinzani nchini kenya Raila Odinga.

Oparanya anahoji kuwa haelewi mbona wakati huu wameamua kumgeuka Raila baada ya kutumia kivuli chake kuweza kushinda viti vya ubunge katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 2022.

“Wapo bungeni kwa ajili ya umaarufu wa Raila Odinga,ni wasaliti ambao hawafai kuwa na sisi,” alisema Oparanya.

Semi za oparanya ziliungwa mkono na katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna ambaye anasema kuwa tayari amewaandikia barua viongozi hao.

Seneta wa kaunti ya Kisumu Tom Ojienda ambaye alikuwa mojawapo wa viongozi kutoka eneo la nyanza waliokutana na Rais William Ruto ikulu Nairobi alidinda kuhudhuria mkutano wa leo wa kisiasa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted