Chelsea Kumenyana Na Dortmund Katika Dimba La UEFA

Kocha mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Edin Terzic amepuuzilia mbali uwezekano wa nyota Jude Bellingham ya kuondoka kwenye kikosi chake wakati klabu hiyo linajiandaa kumenyana na Chelsea...

0

Kocha mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Edin Terzic amepuuzilia mbali uwezekano wa nyota Jude Bellingham ya kuondoka kwenye kikosi chake wakati klabu hiyo linajiandaa kumenyana na Chelsea hii leo kwenye kinyanganyiro cha kombe la klabu bingwa barani ulaya.

Nyota huyo mwenye umzi wa miaka 19 alikuwa nguzo muhimu katika timu ya taifa ya Uingereza katika kombe la dunia na vile vile amechangia pakubwa kwa ushindi wa mechi 10 mfululizo wa Dortmund  msimu huu.

Burusia Dortmund inapania kuionesha Chelsea kivumbi katika dimba hilo litakayo sakatatwa jumaine usiku na Terzic anaamini vijana wake watatoboa kuumiliki na kuzua mashambulizi yeyote kutoka kwa the blues.

Katika awamu ya kwanza, wajerumani waliilaza Chealse Bao moja kwa sufuri.

Mechi ya leo itachezwa katika uwanja wa Stamford bridge jijini london. Huenda recce james akarejea kwa kikosi cha graham potter ambayo imekubwa na wingi wa majereha.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted