Matiang’i Adinda Kuandikisha Taarifa Kwa DCI

Kulikuwa na hali ya mshike mshike katika afisi za DCI baada ya aliyekuwa waziri wa usalama Dkt Fred Matiangi Kudinda kuandikisha Taarifa kwa idara hiyo ya Upelelezi. Badala...

0

Kulikuwa na hali ya mshike mshike katika afisi za DCI baada ya aliyekuwa waziri wa usalama Dkt Fred Matiangi Kudinda kuandikisha Taarifa kwa idara hiyo ya Upelelezi.

Badala yake Matiangi aliamua kusalia kimya na kutangaza kuwa hana la kusema.

Matiangi aliamua kusalia kimya Baaya mawakili wake kumshauri hivyo kwani inakubalika kiseria

Matiangi aliwasili katika afisi hizo Jumanne asubuhi na kufululiza moja kwa moja hadi kwa kitenzo cha upelelezi. Alikuwa  ameandamana na kikosi kizima cha mawakili wakiongozwa na mawakali Otiende Amolo, Okong’o Omogeni, Danston Omari na Steve Mogaka.

“Wapelelezi wanaonekana kupewa muongozo kutoka mahali kwingine ya kutishia kuzuilia Matiangi. Lakini kundi la mawakili wamewaambia wapelelezi kuwa kuna amri ya mahakama inyowazuia kumkamata. Nitazidi kujulisha Taifa kinachojiri hapa ‘’Kasema Mmoja wa mawakili wa Dr Matiangi

.

‘’Kwa sasa kuna njama ya kukaidi agizo la mahakama na kumshika aliyekewa waziri. Lakini tumekita kambi hapa kwa DCI  kuhakikisha haki za Matiangi zinatekelezwa’’ Kaongeza kusema Steve Mogaka

Langoni mwa afisi za DCI, usalama ulikuwa umeimarisha wa kutosha.

Matiangi anatuhumiwa kueneza habari za uongo za kuvamiwa na maafisa wa polisi nyumbani kwake mtaa wa kifahari wa Karena Mnamo tarehe 8 mwezi Februari mwaka huu

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted