Kampeni Ya Kukomesha Kejeli Ya Hedhi Yazinduliwa Kenya

Wanawake wamezindua kampeni inayofahamika kama  #StainNotShame kama njia moja wapo ya kukomesha unyanyapaa dhidi ya hedhi

0

Wanawake wa Kenya hii leo alhamisi tarehe 9 mwezi Ferbruari wamezindua kampeni inayofahamika kama  #StainNotShame kama njia moja wapo ya kukomesha unyanyapaa dhidi ya hedhi kwa akina dada.

Kulingana na shirika moja la kimataifa lisilo la serikali na linalopambana na unyanyapaa dhidi ya hedhi, umeonyesha asilimia 65 ya wanawake nchini Kenya hawana uwezo wa kupata vizodo na vile vile zaidi ya wanafunzi milioni moja nchini hulazimika kusalia nyumbani takribani siku nne kwa mwezi kwa kutokuwa na uwezo wa kupata au kununua sodo ya kuzuia hedhi.

Kwa mjibu wa shirika hilo, wengi wa wasichana wamejitia kitanzi kutokana na ongezeko la mzongo wa mawazo

Kampeni hii inaongozwa na baadhi ya wanamitindo nchini ambao wameamua kupaka rangi nyekundu mbele na yumba ya nguo zao kama njia moja wapo ya kuweka wazi na kuelezea umma kuwa hedhi ni jambo la kawaida.

Kutokana na hayo, wanamitindo hao sasa wanawataka wakenya wote kujitokeza na kuunga mkono kampeni yao. Aidha wanaitaka bunge la kitaifa kupitisha sheria ya kukomesha kejeli dhidi ya hedhi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted