Yanga Yafuzu Robo Fainali Ya Kombe La Shirikisho Afrika

Yanga imeandika Historia baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Kwa mara ya kwanza, mafanikio makubwa waliyokuwa nayo ilikuwa ni kuishia hatua ya makundi.

0

Kennedy Musonda alikuwa nguzo muhimu katika kuhakikisha Yangaimetua salama wa salmini robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kufuatia bao na pasi safi aliyotoa leo, Jumapili dhidi ya Monastir ya Tunisia kwenye Uwanja wa Banjamin Mkapa.

Kufika kwa Yanga robo fainali hiyo kitawafanya kuvuna dola 350,000 za CAF ambazo ni zaidi ya Sh 800milioni.

Musonda aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo, ameendelea kuthibitisha ubora wake akiwa na vijana hao wa Jangwani kwa kuhusika kwenye matokeo muhimu ambayo yanaifanya Yanga kuwa timu ya pili msimu huu kutoka Tanzania kutinga robo fainali ya michuano Kimataifa.

Mshambuliaji huyo Raia wa Zambia aliipa Yanga bao moja kabla ya mapunziko baada ya kufunga dakika ya 33 na kisha kumpakulia pasi nyerezi Fiston Mayele dakika ya 59.

Yanga imeandika Historia baada ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Kwa mara ya kwanza, mafanikio makubwa waliyokuwa nayo ilikuwa ni kuishia hatua ya makundi.

Yanga itamaliza mchezo wake wa hatua ya makundi  dhidi ya TP Mazembe ikiwa ugenini huku ikisaka uongozi wa kundi lake D kwa Sasa wapo pointi sawa na Monastir wakiwa na pointi 10.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuingiza timu mbili kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya CAF, ikumbukwe kuwa Simba ilitinga Jana, Jumamosi baada ya kuishushia mvua ya mabao 7-0 Horoya ya Guinea.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted