Michezo Afrika yakumbwa na madai ya unyanyasaji wa kijinsia nchini DR Congo na Cameroon

Kocha wa zamani wa kandanda nchini DR Congo amesimamishwa kazi kwa muda wa miezi mitano baada ya uchunguzi wa awali wa kamati ya maadili ya Fifa kuhusu tuhuma...

0

Kocha wa zamani wa kandanda nchini DR Congo amesimamishwa kazi kwa muda wa miezi mitano baada ya uchunguzi wa awali wa kamati ya maadili ya Fifa kuhusu tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto wadogo.

Jonathan Bukabakwa alikuwa mmoja wa makocha kadhaa nchini wanaochunguzwa baada ya tuhuma za kutolewa kwenye vyombo kadhaa vya habari mwezi Novemba mwaka jana.

Alikuwa akifanya kazi ya ukocha katika vilabu vya mikoa ya Limpopo na Malebo.

Kusimamishwa kwa Bukabakwa kunahusu shughuli zote zinazohusiana na soka katika ngazi ya kitaifa na kimataifa baada ya taratibu rasmi za uchunguzi kufunguliwa na Fifa hapo jana.

Wakati huo huo, msimamizi mkuu katika soka ya walemavu nchini Cameroon pia amesimamishwa kazi huku uchunguzi ukifanywa kuhusu tuhuma za ubakaji dhidi yake.

Herve Guy Ngoyo Ngong, ambaye amekana madai hayo, ni rais wa moja ya matawi kadhaa ya uongozi chini ya udhibiti wa Kamati ya Olimpiki ya Walemavu ya Cameroon, ambayo imetoa agizo hilo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted