Mandonga Amshinda Mganda Lukyamuzi Kwenye Pigano Kali Jijini Nairobi

Bondia Mtanzania, Karim Mandoga 'Mtu Kazi' amshinda Kenneth Lukyamuzi wa Uganda kwa pointi za majaji wawili baada ya pambano kali la raundi 8

0

Bondia Mtanzania, Karim Mandoga ‘Mtu Kazi’ amshinda Kenneth Lukyamuzi wa Uganda kwa pointi za majaji wawili baada ya pambano kali la raundi 8 lilipigwa siku ya Jumamosi katika ukumbi wa kasarani gymnasium

Mandonga ametwaa ubingwa wa PST uzani wa Light Heavyweight ikiwa ni ubingwa wake wa kwanza tangu aingie kwenye Ndondi miaka 8 iliyopita.

“Nilikuwa na ndoto siku moja nije kutwaa mkanda Hakika allah amesikia kilio changu.” kasema mandonga

Mandonga hata hivyo alionekana kulemewa katika raundi za pili za kwanza lakini akajikakamua katika kipidi cha mwisho mwaisho na kuibuga na ushindi.

Bondia Lukyamuzi ana rekodi ya kushinda mapambano manne kati ya 11 na amepoteza mapambano 6 sare ikiwa ni pambano moja

Mandonga alirejea Kenya kuchuana na Lukyamuzi ikiwa ni miezi mitatu tangu ampasue Mkenya Daniel Wanyonyi kwa TKO katika raundi ya tano mnamo Januari 14, 2023.

katika pigano nyingine zilizopiganwa, Daniel Wanyonyi wa kenya alimpiga knock out Muzamir Kakande katika roundi ya kwanza.

Nick Otieno mwenye umri wa miaka 49 akalemewea na kinda wa Tanzania Hassan Ndonga mwenye umri wa miaka 22.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted