Morocco Yaandikisha Historia Baada Ya Kuibwaga Brazil 2-1

Morocco inakuwa timu ya pili barani Afrika kuwai kuishinda Brazil katika historia ya soka duniani

0

Sofiane Boufal na Abdelhamid Sabiri walifunga na kuipa Morocco ushindi wa 2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil mjini Tangier Jumamosi, na kupata ushindi wao wa kwanza dhidi ya mabingwa hao mara tano wa dunia.

Morocco,ambao walifika nusu fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar 2022, hawakusita na kutwaa   ushindi dhidi ya timu  iliyoorodheshwa ya kwanza dunia na FIFA.

Wakiwa wakishangiliwa na mashabiki 65,000 katika Uwanja wa  Batouta Jijini Tangier, Morocco walijaribu kuanza haraka lakini Brazil walisimama imara na mechi nusura igeuke kuwa ya miereka, kutokana na kile Samba Boys walisema ni usimamizi mbaya wa mechi hiyo ambayo ilisheheni rafu chungu nzima

Brazil walikuwa wakali zaidi na kudhibiti kumiliki mpira huku Morocco wakiwa hatari wakati wote kwenye shambulizi la kustukiza.

Kipa Yassine Bounou nusura aizawadie Brazil bao katika dakika ya 22 kwa makosa ya kuchekesha wakati akijaribu kuuweka mpira kwa miguu yake, lakini shuti la Rony kuelekea lango lilizuiwa na beki na Bounou akafanikiwa kuokoa kwa muda na kumzuia nyota wa Real Madrid Vinicius Junior kutinga bao

Dakika moja baadaye, Bounou kwa mara nyingine alifanya makosa kwa kumpa mpira Vinicius Junior ambaye alitia wazuni mpira, lakini juhudi hizo zilikataliwa na VAR baadaya kusemeka Vinicuius alikuwa ameotea.

Hii ilikuwa mechi ya kimataifa ya kirafiki na Morocco ilitumia mechi hiyo kama ya makaribisho nyumbani tangu kumalizika wa kombe la dunia. Aidha morocco inakuwa timu ya pili barani afrika kuwai kuishinda brazil katika historia ya soka dunia. Cameroon ndio ya kuanza kuifunga brazil, katika kumbe la dunia 2022.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted