Ufanisi Wa Karim Mandonga Wachochea Kuandaliwa Kwa Misusuru Ya Ndondi Kenya

Misururu zaidi ya michezo ya  ndondi yamepangwa kote nchini Kenya kama sehemu moja ya kukuza umaarufu na ushirikishaji  wa jamii katika fani hio.

0

Misururu zaidi ya michezo ya  ndondi yamepangwa kote nchini Kenya kama sehemu moja ya kukuza umaarufu na ushirikishaji  wa jamii katika fani hio.

Kampuni ya mchezo wa Kamari, BetNare, inasema imejitolea kufanya kazi kwa karibu na shiriko la ndondi nchini kenya na wakuzaji wa mchezo huo kwa minajili ya kukuza mchezo wa masumbwi mashinani

Uamuzi huu umefuatia matukio mawili ya ndondi ya kufana yaliyofana kwa muda wa miezi miwili iliyopita katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa KICC mnamo Januari na wa hivi majuzi  katika ukumbi wa Kasarani.

“Tunashauriana na waandalizi wa ndondi ya kimataifa na wakuzaji wa mchezo huo kuona jinsi tunavyoweza kufanya kazi pamoja ili kuwa na spoti  ya ndondi katika maeneo mengine ya nchi,” ilisema kampuni ya BetNare.

“Tumekuwa na ndondi mawili yenye mafanikio makubwa sana jijini Nairobi na ni wazi kwamba basi michezo inapendwa na watu wengi na inazidi Kukua. Sasa tunatakiwa kupeleka matukio mengi zaidi maeneo mengine ya nchi, pia nafurahisha kusikia kwamba Bi  Nancy Matimu (mkurugenzi mkuu wa Multichoice) anapania  kuendeleza michezo huu kwa ujumla’’

“Kampuni ya BetNare imejitolea kusaidia kujenga upya mchezo huo ambao wakati mmoja ulikuwa maarufu sana. Tunataka kusaidia kuibua vipaji vipya na kuwa na mastaa kama Robert Wangila Napunyi…

Mwishoni mwa juma, mapigano kadhaa ya ndondi yalifanyika katika Ukumbi Kasarani

Mtanzania Karim “Mtu Kazi” Mandonga alimbwaga Mganda Kenneth  Lukyamuzi wa Uganda katika uamuzi wa mgawanyiko wa majaji na kutwaa taji la PST.

Kwingineko mkenya Daniel Wanyonyi alimshinda mpinzani wa Uganda Charles Kakande katika raundi sita.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted